MABESTE AMKINGIA KIFUA MAMA WATOTO WAKE : ”WABONGO HAWAKOSI CHA KUSEMA”
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Mabeste
Venance amemkingia kifua meneja na mama watoto wake aitwaye Lisa na
kuwashangaa watu wanaodai kwamba tangu aanze kumenijiwa na mwanamke huyo
imempelekea apotea kabisa kwenye gemu.
Hitmaker huyo wa ”Baadae sana” ameeleza chanzo cha
ukimya wake kimetokana na kuuguliwa na mkewe kwa kipindi kirefu sana
tangu alipojifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume.
”Ukweli ambao sijawai usema nimeuficha kwa mda
mrefu ni huu wife wangu ameumwa mda mrefu sana ever since kajifungua my
son hakua sawa….then hali ikawa mbaya zaid five months ago! So I had to
be there for her,ilifikia stage nikahis I will loose her!” aliandika mabeste kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Mabeste alienda mbele zaidi na kuongeza, ”I lost
my mom nikiwa mdogo I didn’t want the same for my son….mda mwingi
nimeutumia kumuuguza my wife na kucheer na mtoto wangu!! Hapo awali
nlikua napost picha za wife nikisema get well soon na zingine nikiwa
church!! Nlitumia mda wangu kuuguza na nikishinda church kumuomba Mungu!
So kazi zisingeweza kwenda hata kama ningekua Bhits au ningekua na
manager mwingine!! Nilificha nikasingizia vngine but coz lies n rumors
zmekua nyingi lemmi b open to my fans, now Mungu amejibu maombi yuko poa
sana!”.
”Behind every successful Men there is a woman!!
Nisiongee sana kapona acha tuone 2015! Mlio dhani mabeste kaishiwa mimi
mwenzenu ndo kwanza naanza safari….” aliandika mbeste.

No comments:
Post a Comment