BONDIA MUHAMMAD ALI ASUMBULIWA NA HOMA YA MAPAFU
Aliyekuwa
bingwa mara tatu wa uzito wa juu Duniani, bondia Muhammad Ali amepata
nafuu baada ya kulazwa hospitalini alipokuwa akipatiwa matibabu baada
ya kushambuliwa na homa ya mapafu.
Kwa mujibu wa msemaji wa bondia huyo, Bw. Bob Gunnell
aliiambia tovuti ya Daily Mail kwa njia ya simu kwamba Muhammad Ali
amekuwa akipatiwa matibabu na jopo lake la madaktari na hali yake
imeimarika.
”Alikwenda hospitalini asubuhi hii” alisema Gunnel na kuongeza ”alishikwa na nimonia kali na kufanyiwa vipimo vizuri”
Hata hivyo msemaji huyo aligoma kutaja hospitali aliyokuwa
amelazwa bondia huyo kutokana ombi la familia kutaka jambo hilo liwe la
faragha.
Mara ya mwisho Ali alionekana katika Umma mnamo mwezi
Septemba alipohudhuria sherehe katika mji aliozaliwa wa Louisville
kwenye utoaji wa Tuzo za Muhammad Ali Humanitarian.
No comments:
Post a Comment