Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO:Warioba apigilia msumari escrow

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
---
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji
wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa
ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika
uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.
Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake
Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka
katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.
Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa,
wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola
na wizara hizo kuachwa.
No comments:
Post a Comment