UNESCO, SAMSUNG KUJENGA KIJIJI CHA DIGITALI OLOLOSOKWAN
Mwakilishi
mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa
Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo wakibadilishana
nyaraka za makubaliano hayo yaliyofanyika ofisi za UNESCO.
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
limetiliana saini mkataba na kampuni ya elektroniki ya Samsung ya ujenzi
wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo. Makubaliano hayo
yalitiwa saini hivi karibuni kati ya Mwakilishi mkazi Unesco nchini Bi.
Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini
Tanzania, Bw. Mike Seo katika hafla iliyofanyika ofisi za UNESCO.
Kijiji
hicho kitakuwa na shule yenye Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti,
kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye
kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua
kwa ajili ya kijiji hicho.
Utiaji
saini huo ulioshuhudiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya
UNESCO, bi. Leah Kihimbi kutoka wizara ya habari, vijana, utamaduni na
michezo na Dkt. N. Iriya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dar es
Salaam na wafanyakazi wa UNESCO. Katika hafla hiyo Bi. Rodrigues
amesema kwamba mradi huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai
elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji
wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
Baadhi
ya wafanyakazi wa UNESCO na Samsung wakifuatilia kwa umakini hafla hiyo
fupi ya kutiliana saini makubaliano baina ya Samsung Tanzania na
UNESCO.
“Kupitia
kijiji hiki vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo
yao”, alisema Bi. Rodrigues. Naye Mkurugenzi wa Samsung Electronics
nchini Tanzania miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika
mradi huo wa kijiji cha digitali huko Loliondo ni kuweza kupata nishati
rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira.
Alisema
kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa vijiji vya
digitali. Aidha kwa kitendo hicho Afrika inaonesha dunia ni kwa namna
teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa
ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.
Bi
Leah Kihimbi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya habari,vijana,
utamaduni na michezo, alisema kupitia vijiji vya digitali itawezekana
kutekeleza program ya elimu kwa watu wanaoishi Loliondo huku tamaduni
zao zikihifadhiwa.
Kijiji
hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani
Afrika. Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa mjini Zanzibar kwa
ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka 2015.
Pichani ni muonekano wa mchoro wa kijiji hicho utakavyokua.
No comments:
Post a Comment