TANGAZO LA MSIBA WA KEPTENI-SP. KIDAI SENZALA KALUSE

Mrakibu wa Polisi-Captain Kidai Senzala Kaluse enzi za uhai wake.
Familia
ya Mzee Senzala Kaluse wa Kimara Mwisho Dar es Salaam, inasikitika
kutangaza kifo cha mtoto wao KIDAI SENZALA KALUSE kilichotokea Novemba
29, 2014 Saa 4 asubuhi kwa ajali ya Helkopta huko Kipunguni B, Moshi Bar
Dar es Salaam.
Mipango
ya mazishi inafanyika nyumbani kwa baba yake Mzee Kaluse, Kimara
Mwisho. Habari ziwafikie, Ukoo wote wa Warutu, Ukoo wa Kaluse, Ukoo wa
Mroki, Familia yote ya Timothy Nathan, Ukoo wa Kajiru na Taluka, Wakamba
wote wa Ugweno Msangeni, Bibi wa Marehemu Mary Nathan wa Kinyenze-
Morogoro, Familia ya Tarimo ya Ukonga Mombasa, Omary Msuya wa Moshi, Abdalh Mgonja wa Gonja Maore, Hosea wa Arusha.
Taarifa
pia ziwafike maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Kikosi cha
Polisi Anga, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo.
Misa
ya kuaga Mwili wa Marehemu itafanyika mnyumbani kwao kuanzia Saa 6:00
kabla ya safari ya kuelekea Gonja Maore, Wilaya ya Same Mkoani
Kilimanjaro kuanza na mazishi yatafanyika Jumatatu Kijijini Kwao Gonja
Maore.
Mawasiliano zaidi: Mroki Mroki- +255 717002303.
MATAYO 5: 4 HERI WENYE HUZUNI; MAANA WAO WATAFARIJIKA
No comments:
Post a Comment