TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2014 MUSOMA LASITISHWA KUFUATIA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA LEO.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,pichani wa tatu shoto Ruge
Mutahaba akiwa sambamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa
kutumbuiza leo usiku mjini Musoma kwenye tamasha la Fiesta,lakini hata
hivyo Uongozi wa Clouds Media Group,Prime Time Priomotions ambao ndio
waandaaji pamoja na Wadhamini wa tamasha hilo kwa pamoja wamekubaliana
kuahirisha onyesho hilo mpaka hapo baadae itakapotangazwa tena.
Kuaihirishwa
huko kunafuatia ajali mbaya na ya aina yake iliyopelekea simanzi na
majonzi makubwa wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake.Waandaji wa
tamasha hilo pamoja na Wasanii pia walipeleka vifaa mbalimbali kwa ajili
ya kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali
hiyo,Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Mtangazaji
wa Clouds FM,Adam Mchomvu sambamba na Msanii wa muziki wa kizazi kipya
ajulikanae kwa jina la kisanii Shilole sambamba na Mkurugenzi wa Vipindi
na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba wakikabidhi vifaa
tiba mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya awali kwa majeruhi
mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk.Samsoni Winani.
Mganga
Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani akifafanua jambo kufuatia ajali
mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za
usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara
baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA
COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika kijiji cha SabaSaba,nje
kidogo ya mji wa Musoma mchana huu.Ambapo DK Samsoni alisema kuwa ajali
hiyo ni aina yake na haijawahi tokea tangu ajali ya aina hiyo
ilivyotokea mnamo mwaka 1996.
Mkuu
wa Wilaya ya Busega Paul Mzindakaya akimpa pole Mganga Mkuu wa mkoa wa
Mara,Dk.Samsoni Winani kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la
Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa
likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa
uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T
736 AWJ katika katika kijiji cha eneo la SabaSaba,nje kidogo ya mji wa
Musoma mchana huu.
No comments:
Post a Comment