WATU ZAIDI YA 35 WAFARIKI DUNIA KUFUATIA AJALI YA MABASI ILIYOTOKEA JANA MJINI MUSOMA ANEO MAARUFU LA SABA SABA
Basi
la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa
likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeharibika vibaya
baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA
COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini
Musoma mchana huu.
Watu
zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 86
kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi
sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa
likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za
usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza
kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa
kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza
kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia
mtoni.
Hali
iliyoipelekea basi hilo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo
bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo
kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari
hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja
amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
Basi
la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza
linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4
EXPRESS.
Umati
wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya
na kusababisha watu 35 kupoteza maisha hapo hapo,wakishuhudia tukio hilo
la ajali.
Buldoza
likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia
mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na
mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.
Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokoaji ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.
No comments:
Post a Comment