WAZIRI MEMBE AZINDUA FILAMU MPYA YA 'I LOVE MWANZA' JIJINI MWANZA
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akisadiwa na Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, kukata utepe kuzindua
filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone Youth
Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika
hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Mwenyekiti wa
Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza,
Anitha Kagemulo. PICHA ZOTE/ JOHN BADI WA Daily Mitikasi Blog
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akionyesha CD ya
filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth
Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada
ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku.
Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu
kushoto), Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba
(kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania
(TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo.
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akinunua CD ya filamu
mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment
Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua
katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Waziri Membe aliwezesha
filamu hiyo kununuliwa na wadau kwa zaidi ya Milioni 50/- katika hafla hiyo.
Kulia ni Msanii wa Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.
No comments:
Post a Comment