Serikali yapokea msaada wa Helkopta kwa ajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya ujangili
Balozi wa Marekani hapa nchini
Bw. Mark Childress (kushoto) akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Helkopta kutoka kwa Taasisi ya Howard G.
Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren
Buffet (hayupo pichani) kulia ni Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu.Hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt.Idd Mfunda (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa
Kampuni ya Helkopta Charter (EA) Ltd Bw. Peter Achammer wakitiliana saini
katika hati za makabidhiano ya Helkopta moja iliyotolewa kama msaada na Taasisi
ya Howard G. Buffet Foundation ya nchini Marekani.Wanaoshuhudia zoezi hilo ni
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu (aliyesimama kushoto) na Balozi
wa Marekani hapa nchini Mark Childress
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro
Nyalandu akionyesha ufunguo wa Helkopta mara baada ya kukabidhiwa na Afisa
Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helcopter Charter (EA), Peter
Achammer kwa niaba ya Mfuko wa Howard G. Buffet ambapo ni moja ya utekelezaji
wa ahadi za mmiliki wa Mfuko huo alizozitoka kwa Rais Jakaya Kikwete alipofanya
ziara katika Mbuga za wanyama hapa nchini hivi karibuni.Wa pili kulia ni Balozi
wa Marekani nchini, Mark Childress naWaziri Kivuli wa Maliasili na Utalii,
Mchungaji Peter Msigwa .
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amepanda Helkopta
ambayo alikabidhiwa kama msaada kutoka Mfuko wa Howard G. Buffet kwa ajili ya
kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na ujangili.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro
Nyalandu akiteta jambo na Wawakilishi wa
Bunge .katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa Helkopta kwa ajili kupambana
na ujangili nchini Mh. James Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge Maliasili na Mazingira (katikati) na Mhe. Mch. Peter Msigwa
Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Meneja
Mipango na Mikakati wa Howard G. Buffet Foundation Tanzania Chapter Bi.
Ellen Mutalemwa akitoa rai wakati wa hafla ya kukabidhi Helkopta moja
ambayo ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mwenyekiti wa Mfuko huo
alipomtembelea Rais Kikwete hivi karibuni. Helkopta hiyo imetolewa ili
kusaidi juhudi za Serikali katika kupambana na ujangali katika hifadhi
za Taifa.
No comments:
Post a Comment