RAPA COMMON ASAINI MKATABA NA DEF JAM
Rapa aliyewahi kutamba na ngoma ya People maarufu kwa jina la
steji ‘Common’ amesaini mkataba wa kufanya kazi na rekodi lebo ya Def
Jam na Artium huku akiungana na mtayarishaji wa muziki ambaye pia ni
makamu wa Rais wa lebo hiyo aitwae No I.D aliyewahi kufanya nae kazi
kitambo kirefu ikiwemo kwenye albamu yake ya mwisho kuachia ya ‘The
Dreamer/The Believer’ iliyotoka mwaka 2011.
”Najisikia Furaha kushirikiana na No I.D na kuwa sehemu ya
familia ya Def Jam” alisema Common katika taarifa iliyotolewa na Def Jam
huku utaratibu wao wa kwanza kibiashara ukiwa ni kuachia albamu mpya ya
rapa huyo mzaliwa wa Chicago inayokwenda kwa jina la ‘Nobody’s Smiling’
itakayoingia sokoni Julai 22 mwaka huu yenye ngoma kama vile Kingdom
aliyomshirikisha Vince Staples ambayo tayari imekwisha toka. Isikilize
hapo chini
No comments:
Post a Comment