Rais Kikwete akutana na Wataalamu watatu wa utafiti wa chanjo ya malaria kutoka Ifakara Health Institute mjini Malabo, Equatorial Guinea
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo
ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) I
Malabo, Equatorial Guinea) walipomtembelea kwenye makazi yake mjini
Malabo ambako Rais alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa
Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa
tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa
maabara, utambuzi wadudu wa malaria).
Dr
Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa
Ifakara Health Institute (IH) I Malabo, Equatorial Guinea) akifafanunua
jambo kwa Rais Kikwete walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo
ambako, Rais Kikwete alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa
Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa
tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa
maabara, utambuzi wadudu wa malaria).
Picha ya pamoja.Picha na Ikulu
Rais
Kikwete aliwapongeza sana watafiti hao pamoja na taasisi ya IHI kwa
kuiletea sifa Tanzania katika fani ya utafiti nje ya nchi.Watafiti
hao wako Equatorial Guinea (EG) kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo
kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalamu katika utekelezaji wa mradi wa
utafiti wa chanjo ya malaria iitwayo PfSPZ na kuwafunza wenzetu kuhusu
maarifa ya fani hii ya utafiti wa chanjo ya malaria.
IHI
ni shirika la utafiti lenye kufanya tafiti za afya nchini Tanzania
lenye uzoefu wa miaka zaidi ya miaka hamsini. Mfano mmoja wa mafanikio
yake ni utafiti uliopelekea vyandarua vyenye dawa kutumika kama moja
wapo ya njia za kujikinga na malaria nchini Tanzania. Tunafanya
kazi pamoja madaktari na wataalamu kutoka Wizara ya Afya ya EG, shirika
lisilo la kiserikali la Marekani liitwalo MCDI (Medical Care Development
International) na Sanaria ambao ndio watengenezaji wa chanjo hiyo ya
malaria.
Mradi
huu wa utafiti unagharamiwa na serikali ya EG pamoja na sekta binafsi
za mafuta. Mradi huu wa miaka mitano una lengo la kuchunguza kuhusu
uwezo wa chanjo hiyo kukinga dhidi ya ugonjwa wa malaria. Ushirikano huu
ni mmoja ya mfano wa mashirikano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi
ili kutafuta njia bora za kukinga maradhi katika jamii. Vilevile ni
moja ya kielelezo kizuri cha jinsi gani nchi za kusini zinaweza
kushirikiana katika taaluma mbali mbali (south south corporation).
Tumepata
fursa ya kukutana na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshima
Jakaya Mrisho Kikwete Malabo na kumueleza kuhusu kazi tunayofanya na
changamoto mbalimbali zinazotukuta pamoja na kutoa ombi kwa mheshimiwa
Rais kusahilisha mashirikano kati ya nchi mbili za Tanzania na
Equatorial Guinea kupitia Wizara za Afya na Tume za Sayansi na
technologia za nchi hizi mbili. Hili litafanya utelekelezaji wa
mashirikiano hayo kuwa bora zaidi kwa lengo la kunufaisha nchi zote
mbili.
Mashirikiano
haya ni fursa ya watanzania kuwafunza wenzao pamoja na wao kujifunza
kutokana na mashirikiano hayo. Utafiti huo pia utasaidia juhudi za
kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kufanya tafiti zenye lengo la kutafuta
chanjo bora ya malaria pamoja na njia bora za kusambaza chanjo hiyo kwa
nchi zote mbili kama itakuwa ni yenye mafanikio.
No comments:
Post a Comment