Polisi walazimishwa kuishi pamoja Kenya
Kitengo cha utendakazi cha askari polisi Nchini Kenya
kimekumbwa na shida ya ukosefu wa makazi.
Hali imekuwa mbaya sana katika ski za hivu punde kiasi ya kuwa maafisa wa
kike na wenzao wa kiume, wamelazimika kutumia kwa pamoja vyumba vyao
vichache.
Hali inaweza zidi kudorora mwaka ujao ikiwa vyumba vipya havitapatikana kwa haraka kwani maafisa wengine 10,000 wataapishwa kujiunga na Idara ya polisi kuhuidumia wananchi na kulinda usalama .
Mpango huo wa kupanua kitengo hicho, ulizinduliwa bungeni na katibu wa fedha Henry Rotich alipoisoma bajeti ya mwaka 2014/2015, juma lililopita. Kuishi kwenye vibanda
Hii inamaanisha kuwa kurutu anakaribishwa kwa chumba anakoishi Askari na mkewe na familia yake .
“maafisa wengine wanawazuia maafisa hawa wageni kuingia katika nyumba zao na kusababisha hali ngumu kwao.
Maafisa wa polisi watakaokiuka amri hiyo watachukuliwa hatua za kinidhamu . Taarifa hiyo ilisema.
Maafisa waliozungumza na wanahabari, kwa masharti ya kutotajwa walisema kuwa amri hiyo itawanyima faragha na wake zao mbali na kuibua uhasama na ugomvi katika familia zao.
Mgogoro huo uliwalazimisha maafisa hao wapya kutafuta makao katika vibanda viliyo katika vituo vya polisi kwa hofu ya kuvunja nyumba za wenzao .
Maafisa hawa wapya walitawazwa kuwa makonstebo mwezi Aprili na kuchukuliwa katika vitengo vya Polisi ,Kitengo cha Jinai na kikosi cha kupambana na ghasia.
No comments:
Post a Comment