Picha Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Dkt. Mahadhi Juma Maalim Afanya Mazungumzo na Waziri Mwandamizi Anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore,Masagos Zulkifli Ambaye Yupo nchini Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Tano.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi
Juma Maalim (Mb.) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri
Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya
Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi
ya siku tano. Katika mazungumzo yao walisisitiza kuimarisha ushirikiano
katika masuala mbalimbali ikiwemo utalii, uchukuzi na uwekezaji.
Mhe. Zulkifli naye akizungumza wakati wa mkutano wake na Mhe. Dkt. Maalim.
Balozi
wa Tanzania nchini India anayewakilisha pia nchini Singapore, Mhe. John
Kijazi (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na
Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. Nathaniel Kaaya wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Maalim na Mhe.
Zulkifli (hawapo pichani)
Bw. Adam Isara (kushoto), Katibu wa Naibu Waziri na Bw. Khatib Makenga, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo
No comments:
Post a Comment