MARCIO MAXIMO ASAINI MKATABA NA YANGA.
Kocha mkuu wa zamani wa timu ya Taifa, taifa Stars Marcio Maximo
amesaini mkataba wa kuwa kocha mkuu na timu ya Yanga kwa muda wa
miaka miwili. makubaliano hayo yamefikiwa jana, wakala anaye
mwakilisha Ally Mleh wa kampuni ya Manyara Sports Management
amethibitisha hilo.
"Ni
kweli kocha Marcio Maximo amekubali kuingia mkataba na timu ya Yanga
ambapo anatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 27/06/2014 ambapo
atafuatana na msaidizi wake Leonardo Neiva. Mazungumzo ya makubaliano
hayo yalichukua muda mrefu kidogo hatimaye tumefikia
makubaliano.Tunashukuru mungu kila kitu kimekamilika.
Kwa niaba ya Marcio Maximo napenda kuushukuru uongozi wa klabu yaYanga, shukrani za pekee kwa mwenyekiti wa Yanga ndg Yusuf Manji namakamu wake Clement Sanga, kwa kweli wameonyesha umakini naprofessional kwa muda wote wa majadiliano. Nawaombawachezaji,wanachama na wapenzi wote wa yanga tumpe ushirikiano.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars nchini
aliingia mkataba na timu kubwa nchini brazil mpaka mkataba wake
ulipoisha.Kwa wakati huu kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimbali
Zilizotoa ofa nchini China, Ethiopia na Afrika kusini lakini Yanga
wamefanikiwa kumnasa kocha huyo.
Maximo anatarajia kuwasili kesho siku ya Alhamis saa saba mchana
Maximo
ilikuwa awasili nchini baada ya fainali za kombe la dunia lakini
kutokana na mkataba alioingia na Yanga imebidi afupishe mkataba wa kazi
ya 'commentator' aliyokuwa akiifanya nchini Brazil ili awahi kuandaa
program zake Yanga.
No comments:
Post a Comment