FFU wa Ngoma Africa band wapanda tena jukwaani baada ya maombolezo ya msiba wa Iraki Hudu (RIP)
BAADA YA MAOMBELEZO YA KIFO CHA SWAHIBA WAO IRAKI HUDU(RIP)
FFU wa NGOMA AFRICA BAND WAPANDA TENA JUKWAANI UGHAIBUNI !
Frankfurt,Ujerumani.
Bendi
ya Muziki wa dansi Ngoma Africa band alimaarufu "
FFU-Ughaibuni" walipanda tena jukwaani jumamosi ya 21 Juni 2014 katika
Ditzenbach Festival,nje kidogo ya mji wa Frankfurt,kule Ujerumani.
Bendi
hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya yenye makao yake nchini
Ujerumani ilikuwa katika maombolezo ya siku saba kutokana na kifo cha
layekuwa Swahiba wao wa karibu bondia mkongwe hayati IRAKI HUDU aka
Kimbunga(RIP) ambaye alifariki 13.juni 2014 mjini Dar-es-salaam. Baada
ya maombolezo hayo bendi hiyo sasa inaendelea na taratibu zake za
maonyesho huko ughaibuni.
wasikilize ffu-ughaibuni at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment