Header Ads

LULU NA JOTI WAFUNGA NDOA KIMYA KIMYA, USIKOSE KUANGALIA NDOA YAO IFIKAPO SAA 4 USIKU ITV

Hatimaye Msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu afunga Ndoa ya Kimya Kimya na Msanii wa Vichekesho Lucas Mhavile maarufu kama JOTI. Ndoa hiyo ya Kimya imefungwa siku chache zilizopita katika fukwe za Kiota cha Maraha cha Escape 1 Mikocheni.
Mchungaji akiwafungisha Ndoa hiyo ambae pia ana kipawa cha Uchekeshaji na MC aitwaye Mc Pilipili.
Lulu akiwa katika vazi la Harusi kabla hajafunga ndoa hiyo.Ndoa hiyo itarushwa leo Saa Nne usiku katika Kituo cha Runinga cha ITV na Marudio yake itakuwa ni Jumapili saa 10 Jioni na Jumatano saa 5 usiku.
Najua ungependa kujua Ndoa hiyo ya Lulu na kuona jinsi ilivyokuwa usikose leo Saa 4 usiku katika Runinga ya ITV. Picha Zote na Josephat Lukaza

No comments:

Powered by Blogger.