ADY BATISTA WA “THE THORN OF THE ROSE” AKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA SINEMA TAMASHA LA ZIFF 2014
ADY de Batista (30).
ADY
de Batista akisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey
Maqueta mara baada ya kuwasili kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani
Zanzibar. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ADY
de Batista alishuka taratibu katika gari la Noah, akiwa amevalia nguo
nyeupe.Alisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta na
kuingia katika ukumbi wa maonesho ya sinema wa wazi uliopo Ngome
Kongwe kwa ajili ya sinema yake ya O Espinho Da Rosa.
Kutoka
kwenye gari hadi alipopokewa na Mtendaji wa tamasha la Filamu la
Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) Profesa Martin Mhando,unamuona mdada
anayejiamini, mwenye uzuri wa asili na weusi unaong'aa majira ya
magharibi kabisa, kabla ya swala ya insha.
ADY de Batista akiingia kwenye lango kuu la Ngome Kongwe.
Alikuwa
anatembea taratibu kama malkia kushoto akiwawepo meneja Sholey na
Kulia rafiki yake wa kiume Antoine Simonet.Nyuma alikuwapo mdogo wake
Nautenle Batista.
Alipokewa
na Mtendaji wa ZIFF Profesa Martin Mhando ambaye alizungumza kidogo
kuhusu O Espinho Da Rosa (The Thorn Of The Rose) kabla ya kumkaribisha
kuzungumza na wapenzi wa sinema waliokuwa wamejazana pomoni katika
ukumbi wa sinema.
ADY de Batista na Meneja wake wakielekea kwenye jukwaa la ZIFF 2014 kuhutubia.
Kabla
ya kuzungumza kuhusu filamu hiyo ambayo imechezwa na Júlio Mesquita,
mwenyewe Ady Batista, Daniel Martinho, Ângelo Torres na Ciomara Morais,
Ady alishukuru kuwepo Zanzibar na kusema kwamba ndoto yake imetimia,
anashukuru sana.
Sinema
hii ambayo ni saa moja na dakika 37, ni sinema yenye makali yote ya
maisha, mashaka na pia imani zilizojikita vyema katika jamii ambayo
imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment