Header Ads

Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO:Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema vijana 10,500 waliojitokeza hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufanya usaili wa nafasi 70 za kazi katika Idara ya Uhamiaji, ni ishara kuwa bomu la ajira litalipuka muda wowote.


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
---
  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema vijana 10,500 waliojitokeza hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufanya usaili wa nafasi 70 za kazi katika Idara ya Uhamiaji, ni ishara kuwa bomu la ajira litalipuka muda wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya Viwanja vya Bunge, Lowassa alisema Serikali ni lazima ihakikishe inatengeneza ajira kwa kuwa kila mwaka zaidi ya vijana 30,000 wanahitimu katika vyuo mbalimbali nchini.


Wasomi hao wa fani mbalimbali walijitokeza katika uwanja huo Ijumaa iliyopita, kuanzia saa 12 asubuhi wakisubiri kufanyiwa usaili huo.

Lowassa ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali kuchukua hatua kukabiliana na tatizo la ajira na akisema ni bomu linalosubiri kulipuka.

No comments:

Powered by Blogger.