CHADEMA KWAWAKA, WAJUMBE WAKE WA BARAZA KUU NA WANACHAMA WATINGA KWA MSAJILI WA VYAMA NA KWA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUOMBA MBOWE NA SLAA WADHIBITIWE KWA UFISADI.
Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho
wilaya ya Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi
ya Msajili wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama
hicho kwa kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya
Chama.
Wanachama
na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga
kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es
Salaam, leo, kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka
viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha
kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
Yona akisaini kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya
Msajili wa Vyama Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia
kwa Yona ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye
ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
Wanachama waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri
kuwasisha barua yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
Yona akionyesha abarua ambayo baadaye aliikabidhi masijala kwa ajili ya kumfikia Msajili wa vyama
Yona akikabidhi barua yao, kwa Mtunza kumbukumbu Mkuu wa Ofisi ya Msajili wa vyama, Jihadhari Saidi.
Yona akizungumza nje ya Ofisi ya Msajili baada ya kuacha barua yao kwa Msajili wa Vyama
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe
wa Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo akisoma
taarifa yao kabla ya kwenda kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
baadaya ya kutoka kwa Msajili ya vyama.
No comments:
Post a Comment