CFAO YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WAMILIKI WA MALORI YA MERCEDES BENZ NCHINI
Msimamizi
wa ufundi wa Magari aina ya Mercedes Benz kutoka kampuni ya CFAO
Motors Bw. Winner Mushi (wa tatu kushoto) akionyesha matumizi ya kifaa
maalum cha ukaguzi wa Malori ya Mercedes Benz (Star Diagnosis Machine)
kwa baadhi ya mafundi na wasimamizi wa ufundi wa magari ya kampuni ya
Bakhresa Group.
Bakhresa
Group ni mmoja wapo wa wateja wa CFAO Motors ambao wanamiliki malori ya
Mercedes Benz. Bw. Heico Herzog Mtaalamu wa ufundi (Flying Doctor)
kutoka Mercedes Benz Ujerumani,(wa tatu kulia) akisimamia shughuli hiyo
iliyoendeshwa na Bw. Mushi.
Wengine
ni Key Account Manager wa Mercedes Benz, Bw. George Washington (kulia),
Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah
Seif (kushoto), Jarangi Nyabagara ambaye ni fundi wa Mercedes Benz (wa
pili kushoto), na aliyechuchumaa ni Mohammed Shariff Meneja wa Karakana
ya Bakhresa Group.
Na Mwandishi Wetu,
KAMPUNI
ya CFAO Motor Tanzania hivi karibuni imezindua huduma mpya ya “Service
Camp” ambapo chini ya huduma hii wa wamiliki wa malori yanayotengenezwa
na Mercedez Benz watapata huduma ya ukaguzi bure na mafunzo kwa
madereva wao.
Akizungumza
na mwandishi wetu, jijini Dar es Salaam Key Account Manager wa Mercedez
Benz, Bw George Washington amesema kwamba wameamua kuanzisha huduma
hiyo ili kuweza kuwahudumia wamilimi wa magari hayo kwa karibu zaidi.“Mpango
huu utapeleka huduma karibu na wateja na kwa kuwa hapo mwanzo wamiliki
wa malori walikuwa hawapati huduma za matengenezo vizuri barani Afrika,”
amesema.
Amesema
kuwa kuna upungufu katika kuwahudumia wamiliki wa malori ya Mercedez
Benz Afrika na hivyo wameona ni busara kuja na ‘Service Camp’ ili
kuwapeleka wateja huduma za matengenezo na mafunzo kwa madereva wao huko
walipo. Aliongeza kwamba huduma hiyo ya
‘Service Camp’ itakuwa ikitolewa kwa njia mbili tofauti ambazo ni kwenda
kwa mteja na kukagua malori bila gharama yoyote.Amesema
kwamba vile vile chini ya huduma hiyo watakuwa wakitoa mafunzo kwa
madereva wa malori ili waweze kujajua vizuri magari hayo pindi
wanapopata tatizo la kiufundi.
Bw.Washighton
aliongeza kwamba vile vile watakuwa wanawafundisha madereva jinsi
vipuri vya Mercedez Benz vinavyopaswa kuwa ili kuweza kutambua vipuri
bandia kwenye soko la nchini au karakana mbalimbali. “Tunawaonesha
vipuri halisi na vipuri bandia kwa sababu kuna madhara katika kutumia
vipuri bandia ambapo madhara yanaweza yasionekane katika muda wa siku
chache bali huonekana baada ya muda mrefu,”
“Ukianza
kuangalia gharama ya kutengeneza gari baada ya madhara kutokea unakuta
gharama yake ni kubwa kuliko ambapo ungetumia vipuri halisi,” alieleza
Bw Washington.
Alisisitiza
kwamba kwamba hatua ya pili ni kuweka kambi barabarani ambapo malori
mengi ya Mercedes Benz yanapita, hivyo kila ambaye anamiliki lori aina
ya Mercedes Benz na anataka kufanyiwa ukaguzi, hupata huduma hiyo bila
gharama, na hatimaye taarifa kamili zake za ukaguzi kurudishwa kwa
mmiliki wake.
Washington
amesema kwamba kampuni ya CFAO inataka kuwa karibu zaidi na wateja
wake, kwani inataka wateja waone kwamba kuna watu wanaowajali ili
kudumisha na kuimarisha uhusiano kati yao na wateja wao.
No comments:
Post a Comment