REBECA MALOPE AWAKUNA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA,NGELEJA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA
Pichani
kati Mgeni rasmi,Mh.William Ngelleja akizindua albamu mpya ya nyimbo za
injili ya muimbaji Grace Mwikwabe (pichani shoto) na kulia ni
Mkurugrenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaji wa matamasha hayo ya
pasaka na Xmass.
Mgeni
rasmi katika muendelezo wa tamasha la Pasaka,ambaye ni Mbunge wa jimbo
la Sengerema,Mh.William Ngereja akizungumza machache mbele ya umati
mkubwa wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye tamasha
hilo,Ngeleja aliwataka viongozi mbalimbali kuliombea Taifa wakati
likipita katika kipindi hiki kigumu cha mchakato wa kuipata Katiba, na
pia aliwataka Wananchi nchini Kote kuwa watulivu,kwani Mungu ni mwema
mchakato wa kuipta katiba mpya utakwisha tu katiba mpya itapatikana.
Mkurugenzi
wa Msama Promotions,Alex Msama akitoa neno la Shukurani kwa viongozi wa
dini mbalimbali pamoja na wakazi wa jiji hilo waliojitokeza kwa wingi
kwenye tamasha la mwendelezo wa Pasaka,lililofanyika ndani ya uwanja wa
CCM Kirumba hapo jana,Wakati huo huo katika tamasha hilo mgeni rasmi
alikuwa ni Mh.William Ngeleja.
Mwanamuziki Rebecca Malope na skwadi lake zima wakiimba jukwaani ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza hapo jana.
Rebecca Malope akiimba kwa hisia jukwaani
Mambo ya Facebook na Twitter hayo live
Mwimbaji
nyota wa nyimbo za kiroho kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope
akitumbuiza jana jioni katika uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza,ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa tamasha la Pasaka huku likiwa
limebeba kauli mbiu maridhawa kabisa isemayo Tanzania Kwanza,Haki Huinua
Taifa.
Sehemu ya umatii wa watu wakifuatilia tamasha hilo.
Mwimbaji
nyota wa injili hapa nchini Rose Muhando akiwaimbisha washabiki na
wapenzi wa nyimbo za injili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
hapo jana wakati wa mwendelezo wa tamasha la pasaka,ambalo limepokelewa
vyema na wakazi wa jiji hilo.
Wadau
wakiwa kwenye mashine zao wakihakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwenye
tamasha hilo ambalo lilipokelewa vyema na wakazi wa jiji la Mwanza.
Waimbaji
mbalimbali mahiri wakishambulia jukwaa kwa pamoja ndani ya uwanja wa
CCM Kirumba hapo jana wakati wa mwendelezo wa tamasha la pasaka jijini
Mwanza
Mkurugenzi
wa Msama Promotions,Alex Msama akimuongoza mwanamuziki mahiri wa nyimbo
za injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope mara baada ya
kumaliza kutumbuiza ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,Malope
alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzikonga nyoyo za washabiki wa jiji hilo
vilivyo.
Pichani
ni sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza hapo jana wakati wa mwendelezo wa
tamasha la Pasaka.
Mwimbaji
wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya,Sara K akiimba kwa hisia mbele
ya wakazi wa jiji la Mwanza waliolipokea vyema tamasha hilo la
mwendelezo wa pasaka.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili,Grace Mwikwambe akiimba
No comments:
Post a Comment