WATOTO YATIMA WAPATIWA MSAADA
Jinsi
wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa wanaosoma shahada ya sheria mwaka wa
tatu waliadhimisha uhuru wa habari kwa kuwatembelea watoto yatima wenye
shida katika kituo cha Teresia Sister kilichoko Tosamaganga na
kuwakabidhi msaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 1na
kucheza nao (picha zote na Denis Mlowe)
======= ========
Na Denis Mlowe,Iringa
KITUO
cha kulelea watoto yatima na wenye shida cha Teresia Sister kilichoko
Tosamanga mkoani Iringa kimepatiwa msaada wa vitu mbalimbali vyenye
thamani ya shilingi milioni 1 na wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaochukua
shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Iringa(Tumaini)
Akikabidhi
misaada hiyo mkufunzi wa sheria wa chuo hicho Penina Manyanki
akiambatana na wanafunzi hao,alisema kuwa wamehamua kutoa misaada hiyo
kwa watoto hao wenye mahitaji kutokana na kusahalika katika jamii na
kwamba misaada hiyo itawasaidia kuwafanya wafurahi na kutambua jamii
ipo pamoja nao.
Alisema
imekuwa kasumba kwa watu wengi kuwasahau watoto yatima na wanaohitaji
msaada hivyo waliamua kuchangishana wanafunzi wa mwaka wa tatu na
kuwapeleka misaada hiyo kwa watoto hao wenye umri wa miezi miwili hadi
miaka sita wanaolelewa katika kituo hicho.
“Huu
ni mwanzo tu wa kuwasaidia watoto hawa na naomba sana jamii iweze
kuwasaidia watoto hawa misaada mbalimbali watambue kuwa kuna watu wako
nyuma yao na wanawapenda sana na kama unavyoona watoto wamefurahi sana
kuungana na dada na kaka zao “ alisema Manyanki
Aidha
Manyanki aliyataka mashirika na watu binafsi kujitokeza kutoa misaada
kwa watoto hao ili kujengea imani ya kutoona kama wanatengwa katika
jamii inayowazunguka
Manyanki
alivitaja vitu vilivyotolewa kuwa ni pamoja na Sukari,Mchele,Mafuta ya
Kula,Sabuni ya kufulia,unga wa ngano,juisi na maharage kwa ajili ya
kuwasaidia watoto hao.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa kituo Sister Mlezi wa Kituo hicho Sr. Hellen
Kihwele aliwashukuru wanafunzi hao kwa misaada kama hiyo ambayo imekuwa
ikisadia watoto kujikimu katika mahitaji yao ya kila siku.
Sister
Hellen alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa
chakula,madawa,mavazi ambapo aliomba serikali kusaidia kutatua kero hizo
ikiwa ni pamoja na kuwajenga watoto mazingira mazuri ya kuishi.
Alitoa
wito kwa wanawake kuacha tabia ya kuwatupa watoto wasio kuwa na hatia
na kuisababishia jamii malezi ingali wazazi wao wapo na wanaendelea
kuponda raha.
No comments:
Post a Comment