PAUL OKOYE ANUNUA MKOKO MPYA AINA YA JEEP WRANGLER
Baada ya kuachia Video yao mpya ya ‘Taste The Money’
inayofanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya Luninga, Memba anayeunda
kundi la Psquare ‘Paul Okoye’ ameonyesha jeuri ya pesa baada ya kununua
mkoko mpya aina ya ’2014 Jeep Wrangler SUV’ na kuupachika jina la utani
‘New Kid’ .
Hiyo inaonyesha wazi ni jinsi gani sanaa ya muziki
inavyowatendea haki na kuwatajirisha mapacha hao kwani ni miezi mitatu
kupita tangu Peter Okoye anunue gari la kifahari aina ya Bentley GT
toleo la mwaka 2014 lililomgharimu takribani Naira milioni 30 ambazo ni
sawa na milioni 300 za kitanzania.
”Ma new baby on da block. My wifey Anita is really gonna get jealous of my new baby tho. Even Onyinye Mike is getting over-jealous. Hehehe! #Testimony o_o” aliandika Paul Okoye kwenye ukurasa wake wa Instagram….
Mkoko mpya wa Paul Okoye aina ya Jeep Wrengler
No comments:
Post a Comment