MKUTANO MKUU WA MWAKA WA AFDB WAMALIZIKA JIJINI KIGALI
Katibu Mkuu
Dkt.Servacius Likwelile akiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu katika Mkutano uliofanyika
katika ukumb wa Ecobank Jijini Kigali Rwanda. .jpg)
.jpg)
Mh.Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akijadiliana jambo na mmoja wa washiriki wa Mkutano
wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unafanyika Kigali Rwanda. Pembeni ni mwa
Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na msaidizi wa
Waziri Bw.Thomas Mabeba.
Waziri wa
Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkuatno mkuu wa mwaka
wa benki ya maendeleo ya Afrika uliofanyika Kigali Nchini Rwanda.
=========== =====
Na Mwandish wetu- Kigali, Rwanda
Viongozi wa Benki Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
wameahidi kuijenga Afrika itakayoendelea kuwa na umoja, mshikamano na yenye
miundombinu ya uhakika. Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa Benki ya AfDB, Dkt.
Donald Kaberuka alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa 49 wa banki hiyo jijini Kigali,
Rwanda. Rais wa Benki hiyo, Dkt. Kaberuka alisema Benki
itasaidia utekelezaji wa mipango bora ambayo itatokana na majadiliano
yatakayofikiwa kwenye vikao nchi wananchama.
Miongoni mwa vipaumbele vya benki kwa kipindi cha
miaka kumi ijayo ni kujenga mazingira ya kuwa na uchumi imara na endelevu, usimamizi
wa maliasili za bara la Afrika na ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha zaidi wanawake
na vijana katika ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika. Katika kuhakikisha maendeleo ya Bara la Afrika
yanafikiwa kupitia Benki ya AfDB kwa kipindi cha miaka 50 ijayo ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa mpango wa ‘Afrika
50’ ambao utapelekea kuongeza ufadhili wa kiasi cha Dola bilioni 100 ambazo
zinahitajika katika kuimarisha miundombinu ya Bara la Afrika.
Awali katika mkutano uliofanyika kati ya Mkurugenzi wa
AfDB kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu na ujumbe wa Tanzania, Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa
jitihada zake za kuhakikisha Tanzania inatekeleza kwa ufanisi miradi yote
inayofadhiliwa na Benki hiyo.“Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika
ambayo inanufaika na fedha kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika,kwa sasa tuna
zaidi ya miradi 31 ambayo inatekelezwa na AfDB” alisema Dkt.Likwilile.
Mwishoni mwa Mkutano wa Magavana wa Benki, Pia
walipitisha kuanzishwa kwa Mfuko wa Pamoja wa Ukuaji wa Afrika (AGTF), na kiasi
cha dola bilioni 2 zitatolewa na China ili kuwezesha AfDB kukabiliana na
kuongezeka kwa mahitaji ya kikanda kwa nchi wanachama wa benki na wateja wa
sekta binafsi.


No comments:
Post a Comment