TAASISI YA KIVULINI YAANZA VIKAO VYA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI KWA WASAIDIZI WA KISHERIA KATIKA WILAYA ZA SENGEREMA, MAGU, MISUNGWI NA KWIMBA MKOANI MWANZA
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Bw. Ramadhan Maselea kizungumzana Wasaidiziwa Kisheria (hawapo pichani) wilaya ya Sengere macha tathmini ya utendaji kazi wa Wasaidizi wa kisheria chini ya mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu kilichoanza mapema asubuhi.
Baadhi
ya wasaidizi wa kisheria katika wilaya ya Sengerema wakiwa katika kikao
cha tathmini ya utendaji kazi wao kwa kipindi cha robo ya pili ya Mwaka
kwa mradi wa mradi wa msaada wa kisheri ana haki za binaadamu.
Bi
Eunice Mayengela Mwanasheria toka Shirika la KIVULINI akitoa ripoti ya
utendaji kazi wa Mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu kwa
washiriki. Bi. Eunice alisema kuwa Lengo la umoja wa Wasaidizi wa
kisheria ni kuhakikisha unasimamia shuguli zote za msaada wa kisheria
katika wilaya husika, nani kiunganishi cha wasidizi wa kisheria katika
ngazi ya wilaya.
Bi
Eunice Mayongela akisisitiza jambo kuhusu Mkutano wa siku moja
ulifanyika katika wilaya ya Sengerema kwa lengo la kuzungumzia maendeleo
ya mradi na changamoto zinaojitokeza.
Mkurugenzi
wa Shirika la KIVULINI akisisitiza Katika kipindi hiki Kivulini ili
wezakutengeneza vitabu kwa ajili ya kuandikishia shauri, kutolea rufaa
,nakupata mrejesho warufaa kutoka kwa watoa huduma wengine nakugawanywa
kwa wasidiziwa kisheria, Pia Kivulini iliweza kuwatengenezea
vitambulisho wasidizi wakisheria ili waweze kutambulikana kwa urahisi
Zaidi katika jamii zao.
Baadhi
ya Wasaidizi wa Kisheria toka wilaya ya Sengerema wakisikiliza kwa
makini ripoti ya kiutendaji katika wilaya ya Sengerema, Mwanza.
---
Taasisi
isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na kutetea haki za Wanawake,
KIVULINI, yenye makao makuu jijini Mwanza imeanza kufanya vikao vya
tathmini ya utendeji kazi wa wasaidizi wa kisheria kwa robo mwaka wa
pili katika ngazi za wilaya chini ya mradi wa msaada wa kisheria na haki
za binaadamu.
Vikao
hivyo vilivyoanza leo katika wilaya ya Sengerema kwa kukutana na
wasaidizi wa kisheria 25 wanaofanya kazi ya kutatua migogoro ya kisheria
kwa kutoa ushauri na elimu ya kisheria katika vijini vya wilaya ya
sengerema, vikao hovyo vinatarajiwa kufanyika pia katika wilaya ya Magu,
Misungwi na Kwimba zote zipo ndani ya mkoa wa Mwanza.
Kivulini
kupitia mradi wa msaada wa kisheria imetekeleza shughuli mbalimbali kwa
lengo la kuisaidia jamii kupata uelewa wa haki zao za kisheria na pia
kundeleza uwepo wa elimu na ushauri wa kisheria katika maeneo ambayo
mradi unatekelezwa.
Na
juhudi kubwa imewekwa katika kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria kwa
sabaabu wasidizi wa kisheria wanaitajika ili kuiwezesha jamii kuweza
kupata haki hasa wale walioko pembezoni mwa miji. Na kwa kupitia umoja
wa wasaidizi wa kisheria wataweza kutoa elimu kwa wanajamii ili waweze
kujua haki zo za kisheria na matatizo yanayopelekea uvunjifu wa haki na
kuchukua hatua.
Kivulini
Iliwezesha uundwaji wa umoja wa vikundi vinne vya wasaidizi wa
kisheria katika wilaya ya kwimba, Misungwi, Sengerema na Magu na umoja
huo unaundwa na jumla ya wajumbe 25 kwa kila kikundi ambao walipata
mafunzo ya wasaidizi wa kisheria kwa kutumia mtaala wa chama cha
wanasheria Tanganyika.
Wasaidizi
wa kisheria wameendelea kutoa huduma ya ushauri wa kisheria kwa
wanajamii hasa kwa makundi yasiyojiweza katika kata 52, kwa kipindi cha
robo mwaka ya pili wasaidizi wa kisheria wamepokea mashauri 129 kwa
ujumla katika mashauri hayo yaliyokamilika ni mashauri 60 yaliyotolewa
rufaa ni 43 na yanayoendelea nimashauri 43, ukilinganisha na robo mwaka
ya kwanza ambapo mashauri 200 yalipokelewa ambayo inafanya jumla ya
mashauri 329 yaliyopokelewa na wasaidizi wa kisheria.
KIVULINI
ni Shirika linalojishughulisha na Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana
lenye makao yake makuu jijiini Mwanza tangu mwaka 1998.
No comments:
Post a Comment