PICHA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: KIKAO CHA ISHIRINI NA TANO(25) CHA BODI YA TAIFA YA PAROLE CHAANZA LEO JIJINI ARUSHA
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia
Munuo(kushoto) akiongoza kikao cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa
kuachiliwa kwa Parole(kulia) ni Kaimu Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole,
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa (kulia).
Kikao hicho cha siku mbili kimeanza leo Aprili 16, 2014 katika Hoteli
ya Charity iliyopo Jijini Arusha.
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia kwa makini majadiliano
ya Wafungwa watakaoachiliwa na Parole katika Kikao cha Bodi ya Taifa ya
Parole kitakachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Aprili 16 - 17, 2014
katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha(wa kwanza kulia ni
Mjumbe na Afisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Bw. Edgar
Luoga(katikati) ni Mjumbe wa Bodi, Dkt. Joseph Chuwa toka Ofisi ya
Mganga Mkuu wa Serikali(kushoto) ni Bw. Jonas Tarimo, Mjumbe wa Bodi ya
Taifa ya Parole.
No comments:
Post a Comment