MABWENI YA WASICHANA YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VITANDA
Mwalimu
mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa maelezo kwa
mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kuhusiana na mabweni ya
wasichana wa shule hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa shule ya sekondari Mwembetogwa
Mwalimu
mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa taarifa ya
shule kwa wazazi na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwembetogwa katika
mahafali ya 18 ya shule hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akichangisha fedha kwa wazazi kwa
ajili ya ununuzi wa vitanda vya mabweni ya wasichana wa shule ya
sekondari Mwembetogwa. (picha zote na Denis Mlowe)
Na Denis Mlowe,Iringa
SHULE
ya Sekondari ya Mwembetogwa iliyoko katika halmashauri ya Manispaa
Iringa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitanda 160 kwa wanafunzi wa
kike wanaotakiwa kuishi katika mabweni yaliyokamilika katika shule hiyo.
Akizungumza
katika mahafali ya 18 ya kidato cha sita na harambee ya kuchangia
ununuzi wa vitanda iliyofanyika jana katika ukumbi wa shule hiyo Mkuu wa
shule,Kelvin Mlengule alisema upungufu wa madawati umesababisha
wanafunzi wa kike wanaotakiwa kuishi shuleni hapo kulazimika kupanga
katika nyumba za watu binafsi na kuwasababisha wengi wao kujiunga katika
makundi hatarishi na kupata ujauzito.
Mlengule
alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanapata vitanda
kwa ajili ya mabweni ya wasichana ambayo tayari yamekwishamilika huku
wakiendelea na mpango wa kujenga mabweni mengine ya wavulana wa kidato
cha tano na sita shuleni hapo.
Alisema
harambee iliyofanyika katika mahafali hayo wamepata mchango wa zaidi ya
shilingi milioni 10 zikiwemo ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali kati ya
shilingi milioni 15 zinazohitajika kukamilisha upungufu wa vitanda na
milango katika mabweni hayo.
Kwa
upande wake mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christene
Ishengoma (Mb), Mkuu wa wilaya ya Kilolo,Gerald Guninita amewataka
wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya kidato cha
sita nchini kutumia muda uliobaki kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa
kumaliza masomo yao kikamilifu.
“Vijana
wangu ni vyema mkatumia muda huu mchache ulibaki kwa ajili ya kujiandaa
zaidi katika kukabiliana na mtihani wenu mnaotarajia kuanza kuufanya
Mei 5nkwa kuweza kufanya vizuri na kuepuka tabia hatarishi ambazo
zinaweza kuwakosesha maisha mazuri hapo mbeleni “ alisema Guninita
Guninita
alisema maadili waliyofundishwa shuleni hapo ni vema wakayatumie vizuri
kwa kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi na kuepuka vishawishi na tama
za kutaka vizuri kuliko uwezo wao na kuwataka kudumisha suala la
nidhamu na kukataa kutumiwa na wanasiasa hususani katika suala hili
linalo endelea sasa la mchakato wa kupata katiba mpya.
Aidha
Guninita ameongeza kuwa wapo wanasiasa watako fanya mikutano na
maandamano kwa kuwashirikisha vijana na kuwapatia pesa ili kuleta vurugu
kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha amani na maisha yao,hivyo
wahakikishe kuwa hawajihusishi kwa namna yeyote katika vitendo hivyo.
Pia
amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kutoa michango mbalimbali
ya maendeleo katika elimu,na kuacha kuchangia michango mingine isiyo na
tija katika jamii zikiwemo harusi na vipaimara.
Katika
mahafari hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Guninita aliahidi kutoa vitanda
40 vyenye thamani ya shilingi milioni 4.8 ikiwemo ahadi yake ya
shilingi laki mbili na elfu arobaini kwa ajili kununulia vitanda viwili.
Shule
ya Sekondari ya Mwembetogwa ni shule inayomilikiwa na wazazi
ilianzishwa mwaka 1984 wakati huo ikiwa na wanafunzi wa kidato cha
kwanza hadi cha nne pekee na wahitimu waliokabidhiwa vyeti walikuwa 122
kati ya 150 walitarajiwa kuhitimu kidato cha sita.
No comments:
Post a Comment