KINANA AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO MJINI INYONGA WILAYANI MLELE MKOANI KATAVI
Jengo la maabara linalojengwa katika Shule ya Sekondari ya Mtapenda, katika Halmashauri ya Nsimbo, mkoani Katavi
Katibu
Mkuu wa CCM,Kinana akishiriki ujenzi wa mradi wa usambazaji wa maji kwa
wananchi alipokagua mradi wa maji uliojengwa kwa sh. mil. 400 katika
Kijiji cha Mwenge mkoani Katavi.
Katbu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kujenga jengo la maabara ya
Shule ya Sekondari ya Mtapenda, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, wakati
wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
Kinana akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Mtapenda, Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisaidia kufyatua matofali ya
kujengea Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Mlele, mjini Inyonga-
Kinana akimwagilia maji matofali ya kujengea ofisi hiyo
Kinana akiangalia maendeleo ya ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Mwenge, Halmashauri ya Nsimbo, mkoani Katavi-
Nape akizungumza na baadhi ya wanachama wa Shina namba 4 katika Kijiji cha Songambele, Nsimbo
Kinana akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Afya cha Inyonga, wakati wa ziara yake wilayani Mlele.
Mganga
Mkuu wa Kituo cha Afya cha Inyonga, Dk. Adis Koni akimpatia maelezo
Kinana na viongozi wengine wa chama na serikali kuhusu kucheleweshwa kwa
makusudi kituo hicho kukipa hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya.
Ucheleweshwaji huo unafanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Kinana akioneshwa baadhi ya vifaa tiba vya kisasa vilivyotolewa msaada na Mbunge wa Jimbo la Katavi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Inyonga,wilayani Mlele mkoani Katavi mapema jioni ya leo.
No comments:
Post a Comment