Jumuiya ya Watanzania nchini Malaysia yapata Uongozi wao
Jumamosi
ya tarehe 29 March 2014, watanzania waishio na wasomao Malaysia
walikutana katika Ubalozi wa Tanzania na kuunda Jumuiya mpya ya
Watanzania wanaoishi South East Asia.
Uongozi
wa Wana Jumuiya hiyo ambao kwa kuanzia ni Watanzania waliopo Malaysia
wakiwa na Balozi Mpya wa Tanzania,Dr. Aziz Ponary Mlima (katikati) na
maafisa wa Ubalozi. Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo, Katibu Mkuu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Elimu, Waziri wa Jamiii,
Utamaduni na Starehe ikiwa pamoja na Wadhamini wawili.

Picha nyingine ni Watanzania wote kwa pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Malaysia.
Jumuiya
hiyo ilianzishwa Mwishoni mwa wiki,ambayo inajulikana kama " Tanzanian
Diaspora in South East Asia" ambayo itakuwa inawashirikisha Watanzania
wote katika nchi za Malaysia, Indonesia, Thailand, Philippines, Brunei,
Laos na Cambodia.
Picha zaidi zinaweza kuonekana kwenye Ukurasa wa Facebook
Watanzania kutoka maeneo hayo wanaombwa kujiunga ili tuweze kutambuana na itakapokuwa lazima kusaidiana.

No comments:
Post a Comment