Wananchi Rukwa Waunga mkono Serikali Kutenga Bajeti Maalum Kukabiliana Vifo vya Uzazi
ZAIDI ya wananchi 16,828 wa Mkoa wa Rukwa wamesaini
ombi la haki (petition), wakiiomba Serikali kutenga bajeti mahususi ili
kuviinua vituo vya afya nchini viweze kutoa huduma za dharura kwa za
uzazi ikiwemo upasuaji, damu salama, vifaa vya kutosha na wafanyakazi
wenye ujuzi.
Taarifa hiyo imetolewa na Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe wa Uzazi
Salama, Bi. Rose Mlay jana mjini hapa mbele ya mgeni rasmi wa siku ya
Utepe Mweupe ambaye ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid
aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
“Lengo
ni kuhakikisha bajeti ya kutosha inatengwa na Serikali Kuu pamoja
halmashauri ili kuhakikisha kuwa angalau asilimia 50 ya vituo vya afya
nchini vinatoa huduma za dharura za uzazi,” alisema Mlay.
Kwa Upande wake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika ujumbe wake
ameziagiza mara moja halmashauri zote nchini kutenga bajeti ya kutosha
ili kuimarisha vituo vya afya viweze kutoa huduma za dharura za uzazi
ikiwamo upasuaji lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Tamko
hilo lipo katika hotuba ya Waziri Pinda iliyosomwa na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akimwakilisha Waziri Mkuu. Katika
maelezo yake Waziri Pinda alisema vifo vya mama na mtoto baado ni
changamoto nchini hivyo Serikali ina kila sababu ya kukabiliana na
changamoto hiyo.
Aliongeza
kuwepo kwa huduma hizo na watalaamu kwenye vituo vya afya na hospitali
nchini, ni njia pekee itakayosaidia kupunguza vifo hivyo.
“Kila mwaka karibu wanawake milioni sita hupoteza maisha ulimwenguni
kote wakati wa kujifungua, asilimia 50 ya wanawake hawa wanatoka kusini
mwa Jangwa la Sahara na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizo kwenye
ukanda huu."
No comments:
Post a Comment