UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE,RIDHIWANI AITEKA KIWANGWA
Ridhiwani
afanya mikutano mitano ya hadhara na miwili zaidi maalum kwa Wazee na
Vijana wa Kiwangwa,maeneo ambayo mgombea wa ubunge kupitia CCM alifanya
mikutano ya hadhara ni Kijiji cha Msuguru,Mwetemo,Msinune,Bago na
Kiwangwa.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mratibu wa
shughuli za kampeni za ubunge wa jimbo la Chalinze akihutubia umati wa
watu waliofurika kwenye uwanja wa kata ya Kiwangwa.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa Ubunge kupitia
CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwa wananchi wa Kijiji cha Kiwangwa katika
jimbo la Chalinze.
Mratibu
wa Kampeni za CCM Jimbo la Chalinze Nape Nnauye wakicheza muziki kidogo
pamoja na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM wakati wa
kumtambulisha na kumnadi mgombea huyo kwa wapiga kura wa Kiwangwa.
Mgombea
wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akihutubia
mamia ya watu waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM na kusisitiza
tashirikiana nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo.
Umati
wa wakazi wa Kiwangwa wakimsikiliza mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze
kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa
amedhamiria kuinua wananchi wa jimbo hilo kielimu,afya,maji na namna ya
kutatua tatizo la wakulima na wafugaji kuwasaidia vijana na kusisitiza
kuna umuhimu wa kudumisha michezo kwa jimbo la Chalinze.
Meneja
wa Kampeni za Ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Steven Kazidi
akihutubia wakazi wa mji wa Kiwangwa wakati wa mkutano wa hadhara wa
kampeni za kumnadi mgombea ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.
Katibu
wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akihutubia wakazi wa
Kiwangwa wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM.
Mtela Mwampamba akihutupia wakazi wa Kiwangwa na kuwaambia mahusiano mazuri kati ya nchi ya Tanzania na CCM ni makubwa mno.
Msanii Maarufu 'Dokii' akicheza na madansa wake wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge za CCM jimbo la Chalinze .
Vijana wa Boda Boda wakiongoza msafara wa mgombea wa ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kuelekea kwenye mkutano wa hadhara.

Mgombea
wa Ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akizungumza na Bibi Tanazina
Mrisho Mfaume wa kijiji cha Msinune ambapo pamoja na mengi waliyoongea
pia Bibi alielezea furaha yake na kuzungumzia CCM inavyoleta maendeleo
kwa wananchi wake.










No comments:
Post a Comment