Serikali yaipongeza Airtel kwa kuchangia maendeleo ya elimu
Meneja
biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brighton Majwala akimkabidhi
vitabu vya sayansi kwa mkuu wa wilaya Arusha John Mongela kwa ajili ya
shule ya sekondari Naura ya jijini Arusha vilivyotolewa na kampuni ya
simu za mkononi ya airtel chini ya mpango wake wa Shule Yetu.
Mkuu
wa wilaya ya Arusha John Mongela akimkabidhi vitabu mbalimbali mkuu wa
shule ya sekondari Naura Sunday Mushobozi vilivyotolewa na kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika shuleni
hapo.
Wanafunzi
wa shule ya sekondari naura ya jijini Arusha wakiangalia vitabu mara
baada ya kukabidhiwa vitabu hivyo na kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel Tanzania.
Mkuu
wa wilaya ya Arusha John Mongela aliwashukuru Airtel kwa msaada wa
vitabu kwa shule ya sekondari ya Naura na kusema kuwa licha ya kuwa ni
jukumu la Serikali kutoa vitabu kwa shule lakini imekuwa ikizidiwa na
majukumu mengi hivyo kwa msaada huo Airtel wanapaswa kupongezwa kwa
kutimiza wajibu wao kwa jamii.
Kauli
hiyo imetolewa wakati Airtel ilipotoa msaada wa vitabu kwa Shule ya
sekondari ya Naura mkoani Arusha chini ya mpango wake maalumu wa “shule
yetu” ambapo Mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana John Mongela alikuwa mgeni
rasmi.
Bwana
Mongela alisema “Vitabu ndio nyenzo ya msingi ya kupata maarifa hivyo
kwa Airtel kujikita katika kusaidia jamii kupitia vitabu kwa shule za
sekondari kutawawezesha wanafunzi na jamii kupata hazina kubwa ya
maarifa na mbinu za kujikwamua kiuchumi kupitia vitabu hivi. Napongeza
sana jitihada hizi na mpango huu ambao ni endelevu na yenye kugusa shule
nyingi na jamii kubwa ya watanzania kwa ujumla”.
Meneja
biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala akizungumzia
msaada huo amesema mpango huo unaolenga kutoa vifaa vya kufundishia
mashuleni yaani vitabu vya hisabati, physikia, chemia na biologia una
lengo la kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni, tunayofuraha
kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari Naura kwani tunaamini
wanafunzi wengi zaidi watanufaika na kuhamasika kujiunga na kusoma
masomo ya sayansi
Kwa
upande wake mkuu wa shule hiyo Gasper Mushobozi aliwashukuru Airtel kwa
msaada huu wa vitabu vya sayansi shuleni hapa , lakini alibainisha kuwa
msaada huu pia uendelezwe kwa kutuboreshea maabara ya shuleni hapo ili
kuweza kupata tecknologia ya sayansi kikamilifu.



No comments:
Post a Comment