Header Ads

SAMSUNG TANZANIA YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI WALIONUNUA BIDHAA HALISI ZA SAMSUNG TANZANIA


Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Samsung Tanzania, Bw Ibrahim Kombo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wa kinyanganyiro cha Promosheni ya E-warranty inayoendeshwa na Kampuni ya Samsung Tanzania, Mteja anayenunua Bidhaa yoyote kutoka Samsung Tanzania atajisajili katika mfumo wa E-warrant ambapo itachezeshwa bahati nasibu na washindi kupatikana.
Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Samsung Tanzania (Kulia) akimkabidhi zawadi ya Microwave, Ndugu Joseph Gobson Nswila mara baada ya kuchaguliwa kuwa mmoja wa mshindi wa promosheni ya E-warrant inayoendeshwa na Kampuni ya Samsung Tanzania
Mshindi wa zawadi ya Home Theater kutoka Samsung Tanzania, Bw John Macharia akipokea zawadi yake kutoka kwa Mhasibu wa Samsung Tanzania, Bw Ibrahim Kombo wakati wa makabidhiano ya zawadi kwa washindi wa promosheni ya E-warranty, Makabidhiano hayo yamefanyika katika Duka la Samsung lililopo Katika Jengo la Quality Center, barabara ya Nyerere Road.
Baba Mzazi wa Lugano Msokwa, ambae amemwakilisha mwanae, Lugano Msokwa ambae amejishindia zawadi ya Simu aina ya Samsung Galaxy Tab 10.1 kutoka Samsung baada ya kununua simu halisi na kuingia kwenye bahati nasibu.
Mshindi Wa Runinga kutoka Samsung Tanzania, Bw Khalil Sherali akipokea zawadi yake ya Runinga kutoka kwa Mhasibu mkuu wa Samsung Tanzania, Bw Ibrahim Kombo wakati wa makabidhiano ya zawadi za washindi wa promosheni ya E-warrant kutoka Samsung Tanzania yaliyofanyika katika Duka la Samsung lililopo Katika Jengo la Quality Center, lililopo Katika Barabara ya Nyerere, Jijini Dar Es Salaam.
Washindi wa Promosheni ya E-warrant inayoendeshwa na Kampuni ya Samsung Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kukabidhi zawadi hizo.
Mmoja wa Washindi wa Runinga Kutoka Samsung Tanzania, Bw Khalil Sherali akiongea na waandishi wa habari  (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Runinga kutoka Samsung Tanzania

No comments:

Powered by Blogger.