Malaysia yazidisha kasi kutafuta Ndege
Ndugu wa waliopotea wameelezwa kuwa wakae tayari kupata habari mbaya
Zoezi
la kutafuta ndege ya abiria ya Malaysia limeendelea kushika kasi baada
ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za
watu waliopotea wakiwa katika ndege hiyo.
Mamlaka
nchini Malaysia zinasema wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji, mara
mbili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa
ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.
Mkuu
wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari
kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50
za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.
Ndege
iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna
dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.Chanzo
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment