PICHA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA:MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) WILAYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA

Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akifungua rasmi Mkutano wa wadau
wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya jana Mjini Matai.
Katika salamu zake za ufunguzi alizitaka halmashauri Mkoani Rukwa
kuhakikisha kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyake vyote vya maamuzi, Aidha
alizitaka Halmashauri ziandae utaratibu wa kuzitambua familia zisizo na
uwezo wa kuchangia na zitenge fedha kutoka katika vyanzo vyake ili
kuzilipia familia hizo na kuhakikisha kuwa hakuna mkazi wa Halmashauri
husika anapoteza maisha kwa kukosa fedha za kuchangia katika Mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF). Mwanachama wa mfuko huo anatakiwa kuchangia Tsh
10,000/= kwa mwaka ambao ni mchango wa kaya moja isiyozidi watu sita

Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo (NHIF) wakiwa katika Mkutano wa kujadili umuhimu wa wa huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na kuangalia namna ya kuzindua rasmi mpango wa kuchangia kabla ya kuugua katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
No comments:
Post a Comment