NMB YAPIGA HODI KWA WAKAZI WA BUZURUGA
NMB yazindua rasmi tawi la Buzuruga mkoani Mwanza .Tawi hili likiwa ni
tawi la tisa kuzinduliwa katika mkoa wa huo huku NMB ikiendelea kuwa ndo benki
yenye matawi mengi zaidi Tanzania.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya wa Nyamagana, Bw. Baraka Konisaga akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB
Buzuruga. wakishuhidia uzinduzi huo kutoka
kushoto ni Naibu Meya Jiji Mwanza mhe. John Minja, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Bw.
Halifa H. Hida na kutoka kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Bw. Straton
Chilongola, Meneja Tawi la NMB Buzuruga, Gadiel Sawe na Meneja Mawasiliano wa
NMB , Josephine Kulwa.

Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,
Mh. Baraka Konisaga ameipongeza benki ya NMB kwa hatua nyingine iliyopiga kwa kusogeza zaidi huduma kwa wateja na kuitaka iendelee kuwa kinara wa huduma za kibenki
nchini. Aliwahamasisha wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi waitumie fursa
ya kuwepo kwa tawi la NMB Buzuruga kukidhi mahitaji yao ya kibenki. Vilevile,
aliwasihi wananchi waache kuweka fedha kwenye chaga za vitanda na badala yake
watumie njia salama ya kuweka fedha benki.

“Ni matumaini yangu kuwa uwepo wa tawi
hili la Buzuruga ni neema kubwa kwa wakazi wa Mabatini, Buzuruga, Nyakato,
Igoma, Kishili, Buswelu na hadi Kisesa hasa wafanyabiashara katika hizi mashine
za mpunga kwani kesi za watu kuporwa fedha majumbani au maofisini zitapungua
badala yake ongezeko la wateja wanaofungua akaunti ndio itakua habari ya eneo
hili” alisema Konisaga.

Kikundi cha Bujora kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi
huo.
huo.
Kwa upande wake, Bw. Straton Chilongola, ambae
ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, alisema “Tangu
kuanzishwa kwa tawi hili tumeshuhudia wakazi wengi wa wakija kufungua akaunti na
kutumia huduma za benki hii. Hii ni uthibitisho kuwa wakazi hawa walikua na kiu
ya kupata huduma za kibenki karibu kariba na milangoni kwao. Lakini pia tutaendelea kubuni mbinu mbalimbali zitakozotuwezesha
kuwafikia wateja wetu karibu zaidi ili kuondoa msongamano kwenye matawi na pia
kuokoa muda wa wateja ili waweze kutumia muda wao kwa shughuli endelevu.”

Tawi hili la Buzuruga, linatoa huduma zote za
kibenki, ikiwa ni pamoja na huduma ya mikopo ya aina mbali mbali bila kusahau
mikopo ya Kilimo. Tawi hili litakua wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa
kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na jioni ( 2:30 asubuhi - 10:00 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili
na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30 asubuhi - 6:30 mchana),
Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.

NMB daima benki
yako!
yako!

No comments:
Post a Comment