MWENYEKITI WA VIJANA CHADEMA NA VIJANA MIA MOJA KATA YA ORTURUMENTI WILAYA YA ARUMERU WAHAMIA CCM
picha
ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wakila kiapo,
katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti
Thomasi Kivuyo.
Mwenyekiti
wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa
siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm
Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla
ya wananchi 100 wa kata ya Ortumunti wilayani Arumeru kutoka katika
vyama mbalimbali vya upinzani wamehamia chama cha Mapinduzi akiwemo
mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA wa kata hiyo .
tukio
hilo limetokea mwishoni mwa wiki,wakati wa mkutano wa hadhara wa
CCM,uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru
mkoani hapa.
Akiongea
wakati wa kurudisha kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya
CCM,Mwenyekiti wa
vijana wa CHADEMA, Thomasi Molel alisema kuwa
ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kubaini kuwa tangu awe mfuasi
wa cha hicho (CHADEMA),Hajapata faida yoyote wala hajaona kitu ambacho
wananchi
wanafaidika kupitia chama hicho.
Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia
katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo, hivyo ameamua kuondoka
katika chama hicho kwani CHADEMA ni chama ambacho hakina demokrasia ya
kweli ambayo inatakiwa iwenacho kama
chama
Alisema kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wamekuwa wanatoa
ahadi za uongo kwa wananchi na mbali ya hivyo pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa
anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atakaeweza
kukisemea chama .
Aidha alibainisha kuwa katika kata yao tangu upinzani wameingia madarakani hamna
kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha
wananchi hela nyingi bila kufanya
maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa
kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea
shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa
Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato
na matumizi ya kata yao tofauti na
kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.
Kwa upande wake
katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na
pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na
matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda
katika ofisi ya mkurugenzi kufuatilia
swala hili.
Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi
kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya
kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka na kata yao haitapata viongozi wazuri.
Aliongeza kuwa haiwezekani kuchagua viomgozi waizi maana
mwisho wa siku wanaoumia ni wao wananchi kwani viongozi wao watakula fedha zao
na wao wataendelea kufaidi huku wao wakiwa wanaendelea kuumia ukuwengine watoto
wao wakilala njaa.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment