Header Ads

MBEYA WAANZA KUNEEMEKA NA MPANGO WA MAENDELEO WA MIAKA MITANO



 Kiongozi
wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) akipata maelezo ya
maendeleo ya Mradi wa Maji ya Mtiririko Kijiji cha Igurusi kutoka kwa
Mshauri wa Mradi huo Mhandisi Kimambo.
 Wakaguzi walipata bahati ya kujionea chanzo cha maji hayo kutoka nje kidogo ya Kijiji cha Igurusi.
 Kikazi Zaidi.. Timu
ya ukaguzi pia ilikagua maendeleo ya Tanki la kuhifadhia maji la mradi
huo. Pichani, Kiongozi wa Ukaguzi, Bibi Florence Mwanri akipanda ngazi
kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa Tanki.
 Ujenzi unaendelea.. Mafundi
wakiendelea na kazi ya ujenzi huku wakaguzi hao wakikagua. Tanki hilo
lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita laki tano ambalo limeshakamilika kwa
asilimia 90. Hadi kukamilika kwake Mradi utagharimu jumla ya Shilingi
zaidi ya Milioni 830.
 Naibu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (Uchumi Jumla), Prof. Longinus
Rutasitara (Aliyenyanyua Mkono) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa
Mradi wa Maji wa Iwalanje wakati Timu ya Ukaguzi ilipotembelea Mradi
huo.
 aonja Maji..
Kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye nguo nyeusi) akionja maji
kutoka moja ya njia za kusambazia maji ya Mradi wa Maji wa Iwalanje.
Kukamilika kwa Mradi huo kumetoa suluhisho la adha ya muda mrefu
iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa Kijiji cha Iwalanje na Taasisi
mbalimbali za Serikali zinazohudumiwa na Mradi huo.

No comments:

Powered by Blogger.