Maalim Seif atembelea na kukagua miradi mitatu Uwanja wa Ndege
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia
ramani ya ujenzi wa miradi mitatu ya uwanja wa ndege wa Zanzibar,
alipofanya ziara ya kutembelea miradi hiyo.
Mtathmini
wa viwango vya ujenzi wa miradi hiyo Bw. Mohd Juma, akitoa maelezo
mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na ujenzi huo.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka Frederick Nkya akionyesha ramani ya ujenzi huo.
Meneja wa mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria bw. Ibrahim Zhang, akimueleza Maalim Seif hatua zinazoendelea za ujenzi huo.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Miundo mbinu
na mawasiliano, viongozi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar pamoja na
wakandarasi wa miradi ya ujenzi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
(picha na Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad OMKR
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea
kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi mitatu
inayoendelea kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Miradi
hiyo inahusisha ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa
kuruka pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege, ujenzi wa uzio wa eneo la
uwanja wa ndege, pamoja na ujenzi wa jingo jipya la abiria (Terminal 2).
Akizungumza
katika ziara ya kutembelea miradi hiyo huko uwanja wa ndege wa
Zanzibar, Maalim Seif amesema hatua iliyofikiwa inatia moyo, na kuwataka
wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati.
Amesema
Serikali kwa upande wake itaweka mkakati wa makusudi ili iweze kumaliza
kuwalipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa, na kuruhusu ujenzi wa
uzio uweze kukamilika kwa akati.
No comments:
Post a Comment