Header Ads

Balozi Mulamula awapongeza Tano Ladies katika siku ya wanawake Duniani







Na Abou Shatry Washington DC

Katika sherehe ya kuadhimisha Siku ya kimataifa ya wanawake duniani,
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula
amewapongeza Tano Ladies kwa uwezo wao mkubwa wa kufanikisha wito wao
wa kuwaweka pamoja wanawake wa Tanzania pamoja na kusherehe
International Women’s Day (IWD) siku ya March 8 inayosherehekewa kila
mwaka ulimwenguni.




Balozi wa Tanzania Marekani na
Mexico Mhe. Liberata Mulamula wa tano kutoka kulia akiwa na kundi zima
la wajasirimali pamoja na Tano Ladies waliopiga goti pichani wakiwa
kwenye sherehe za wanawake duniani aliyoandaliwa rasmi na Tano Ledies
Siku ya Jumamosi Murch 8, 2014 ndani ya ukumbi wa Hampton Inn uliopo
College Park Maryland Nchini Marekani




Na pia kuweza kuwakusanya wanawake wajasirimali wa Tanzania kutoka
sehemu mbalimbalina kwa kuweza kuonyesha ujuzi wao na kuweza
kusherehekea sherehe hizo zinazofanyika kila Mwaka, March 8 duniani
kote.




Balozi Liberata Mulamula aliaaza kwa kuwapongeza na kuwahamasisha
kundi zima la Tano Lades kwa kazi nzuri waliofanya kwa ushirikiano na
wanawake wenziwao wenye kuleta umoja na mshikamano katika kuendeleza
maendeleo katika jamii ya waTanzania waliyopo hapa Amarekani.




Katika sherehe hizo Mhe Mulamula alikutana na wanawake
wajasirimali mbali mbali waliweza kuweka meza zao ndani ya ukumbi na
kutembelea meza moja baada ya moja na kupata maelezo ya kila mjasirimali
katika biashara nazozifanya.




Balozi Mulamula liendelea kwa kuwasifu wanawake wajasirimali
wakitanzania na kuwakabidhi vyeti katika siku hiyo adhimu ilioandaliwa
rasmi na Tano Ladies.




Sherehe hizo zilitumbuizwa kwa nyimbo na wasichana waTanzania
kutoka kwa Mama Jessica Kamala Mushala, pamoja na kundi zima la
Taratibu Youth Association, kutoka Mount Rainier Maryland, na muimbaji
Erica Lulakwa Glenn mTanzania kutoka San Francisco California, katika
sherihe hizo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Humton in College park
Maryland nchini Marekani.








Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula
akipata maelezo mafupi  ya afya kutoka kwa Herriet Shangiraifupi wa
Nesiwangu,bofya hapa kutembelea blog yake nesiwangu.blogs 








Mhe. Liberata Mulamula alipotembelea meza ya Nashona Bibie Lilian Danieli kutoka North Carolina






Mjasirimali Maria Mohamed alipokua kwenye meze yake ya Bahari Deco
Crafts Style the Swahili way kwenye sherehe za wanawake duniani
aliyoandaliwa rasmi na Tano Ledies Siku ya Jumamosi Murch 8, 2014 ndani
ya ukumbi wa Hampton Inn uliopo College Park Maryland Nchini Marekani






Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula
akipata maelezo mafupi kutoka kwa mbunifu wa mishono ya Madira Salha
Mwamende pamoja na familia yake siku ya kimataifa ya wanawake duniani.






Mtuzi wa kitabu cha Taste of Tanzania Miriam Rose Kinunda akiweka
saini kwenye kitabu cha mteja alienunua kwenye maadhimisho ya Siku ya
mwanamke duniani. 






Mtaalamu wa matatizo ya mitandoa (Computer Super Technician) Bi
Mamina Yas akiwa katika utambulisho wa meza ya ujasirimali mwanamke
anaweza kushuhulikia matatizo ya computer yako wakati wowote pale
inapopatwa na matatizo ndani ya maeneo ya DMV unaweza kuwasiliana nae
kama mkaazi wa maeneo haya. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)

No comments:

Powered by Blogger.