Zogo baada ya Msikiti kuvamiwa Kenya
Polisi na vijana waisilamu wamekabiliana Mombasa baada ya tukio la Jumapili
Vijana
walioghadhabishwa na tukio la polisi kuvamia msikiti mmoja unaotumiwa
na wahubiri wanaosemekana kuhubiri itikadi kali za kiisilamu mjini
Mombasa,Pwani ya Kenya, wamekabiliana na polisi kwa siku ya pili leo.
Duru
zinasema kuwa Maafisa wa usalama wanakutana kujadili matukio ya Jumapili
mjini Mombasa ambapo polisi waliwakamata vijana katika msikiti wa Musa .
Waliokamatwa walifikishwa mahakamani kujibu makosa ya kujihusisha na ugaidi.
Msako wa polisi ulisababisha vifo vya watu watatu akiwemo polisi mmoja huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Polisi
walichukua muda wa masaa tatu kuendesha msako, katika msikiti wa Musa
mtaani Majengo baada ya kupata habari kuwa mkutano wa vijana kuhusu
jihad ulikuwa unaendelea ndani ya msikiti huo.
Zogo
lilianza baada ya vijana waliokuwa ndani ya msikiti huo unaohushwa na
marehemu Aboud Rogo kuzuia polisi kuingia ndani. Watu watatu waliuawa na
wengine kujeruhiwa wakati polisi wakifanikiwa kuwakamata vijana karibu
miamoja.
Miongoni
mwa waliokamatwa alikuwa mwanawe marehemu Rogo aliyesema kuwa wakati
walipokamatwa kulikuwa na bunduki 18 ndani ya msikiti huo na kuwa
alihadaiwa kuhudhuria mkutano huo.
Taarifa
zinasema kuwa mkutano huo wa vijana uliandaliwa kupitia mitandao ya
kijamii huku vijikaratasi vikisambazwa mjini humo kuwaalika watu.Chanzo
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment