Picha ya pamoja
KAMPUNI
ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari imeaandaa
mafunzo kwa vijana wanaochoma nyama katika Mabaa yatakayowawezesha
kuingia katika mashindano.
Akizungumzia
lengo la kutoa mafunzo kwa waandaaji wa Nyama choma kwenye mabaa,
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Mbeya na Rukwa,
Cloud Chawene, alisema kampuni imegundua kuwa wamiliki wa baa
wanategemea Nyama kama moja wapo ya vitu vya kuongeza mapato yao.
Alisema
kutokana na hali hiyo wakaona ni vema wakaendesha Semina kwa wachoma
nyama ili waweze kukidhi vigezo vya mahitaji ya Wateja ili waweze
kufurahia Nyama choma kama ilivyo kwa vyakula vingine ili kuendana na
kauli Mbiu ya Bia ya Safari isemayo“ Safari Lager bila nyama choma
haijakamilika.”
Aliongeza
kuwa baada ya mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Baa 42 ambao wametunukiwa
vyeti vya ushiriki pia kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo
washindi 10 watapatikana kutokana na watakaofuzu vigezo na masharti
waliyopewa katika semina hiyo.
Alisema
Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 3, Mwaka huu katika Viwanja vya
Shule ya Msingi RuandaNzovwe ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia
mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni moja, mshindi wa
pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na
Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku mshindi wa Sita hadi wa Kumi
watajinyakulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/=.
Alisema
namna ya kuwapata washindi ni kutokana na wateja kupiga kura katika
utaratibu utakaobandikwa katika Baa shiriki ambapo mteja atapiga kura
kupitia simu ya mkononi ili kuichagua baa inayochoma nyama vizuri.
Aliongeza
kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika katika Mkoa wa Mbeya itaendelea
katika Mikoa mingine ambayo ni Mwanza, Kilimanjaro,Arusha na Dar Es
Salaam mikoa ambayo imetajwa kuwa ndiyo vinara wa uchomaji nyama pamoja
na kuongoza kwa mauzo ya bia ya Safari tofauti na maeneo mengine.
Kwa
upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence P. Salv ambaye pia ni
Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya
kutoa Elimu.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment