PICHA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: HAFLA YA KUMUAGA RASMI KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI NAMIBIA ALIYESTAAFU KWA MUJIBU WA SHERIA YAFANA, WINDHOEK NAMIBIA

Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu Evaristus Shikongo (amesimama
katika Jukwaa) akitoa hotuba fupi mara baada ya kukabidhi rasmi Madaraka
ya Uongozi wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia kwa Kamishna Jenerali
Mpya wa Jeshi la Magereza Raphael Hamunyela.

Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu wa Namibia, Evaristus Shikongo
akiwa ameshika Saa ya Ukutani aliyokabidhiwa na Naibu Kamishna wa
Magereza Mstaafu, John Nyoka(kulia) ambaye alifanyanae kazi Nchini
Namibia kama Mtaalamu wa masuala ya Uendeshaji wa Programu za
Urekebishaji Magerezani kutoka Jeshi la Magereza Tanzania kufuatia
Makubaliano Maalum na Serikali ya Tanzania(kushoto kwa Jenerali) ni Mke
wa Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu wa Namibia.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja (kulia)
akitoa hotuba fupi wakati wa hafla ya kumuaga rasmi Kamishna Jenerali
wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo ambaye amestafu Utumishi
wake wa Umma kwa mujibu wa Sheria.

Baadhi ya Wageni Waalikwa mbalimbali wakiwa katika Hafla fupi ya kumuaga
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo ambaye
amestaafu rasmi Utumishi wake wa Umma kwa mujibu wa Sheria. Sherehe
hizo zimefanyika Februari 01, 2014 katika Ukumbi wa Chuo cha Maafisa
Magereza Omaruru nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia( katikati
meza ya kwanza) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John
Casmir Minja.
Wasanii wa Bendi ya Jeshi la Polisi Nchini Namibia wakitumbuiza mbele ya
Wageni Waalikwa(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi
aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia kufuatia kustaafu
kwakwe Utumishi wa Umma. Sherehe hizo zilizofana sana zimefanyika
Februari 01, 2014 katika Ukumbi wa Chuo cha Maafisa Magereza cha Omaruru
kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja akiwa
katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali Mpya wa Jeshi la Magereza
Nchini Namibia, Raphael Hamunyela(wa pili kushoto), Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini Namibia ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria,
Evaristus Shikongo(wa pili kulia), wa kwanza kushoto ni Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini Uganda.Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment