Header Ads

JACKSON KISWAGA ASIMIKWA RASMI KUWA MLEZI WA CHIPUKIZI WILAYA YA IRINGA VIJIJINI ,ASAS ATOA NENO AKABIDHI MTAJI WA MILIONI 3 KWA UVCCM

Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas wa piki  kulia akimuapisha  mlezi wa  chipukizi  wilaya ya Iringa Bw Jackson Kiswaga  ambae ameteuliwa kushika nafasi hiyo leo 
kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw Asas kulia  akimvisha kofia ya ulezi wa chipukizi Bw Jackson Kiswaga  leo 
Bw Kiswaga  akikabidhiwa vitendea kazi na kamanda wa UVCCM mkoa Bw Salim Asas mara baada ya  kuapishwa kuwa  mlezi wa chipukizi  wilaya ya  Iringa vijijini leo 
Hapa Bw Kiswaga  akiondoka baada ya  kukabidhiwa rasmi ulezi wa chipukizi wilaya ya Iringa vijijini 
Mlezi wa chipukizi wilaya ya Iringa vijijini Jackson Kiswaga kulia akiwa na kamanda wa UVCCM wilaya  hiyo DC wa pangani Bi Hafsa Mtasiwa 
Mlezi wa Chipukizi wilaya ya Iringa vijijini Jackson Kiswaga   akikabidhi  pikipiki kwa chipukizi wilaya  hiyo huku viongozi mbali mbali wakishuhudia 
........................................................................................................................................


KAMANDA  wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri  Asas  amemwapisha  mdau  wa maendeleo  katika jimbo la Kalenga Bw  Jackson   Kiswaga  kuwa mlezi  wa  chipukizi katika  wilaya ya  Iringa    huku Bi Afsa Mtasiwa  akikabidhiwa  mikopo ya Arif Abri  katika nafasi ya ukamanda wa UVCCM wilaya  hiyo bila hata ya kamanda aliyemaliza muda  wake  kushirikishwa katika hafla  hiyo.


Tukio  la  kuwaapisha  viongozi hao  wa chipukizi na kamanda  wa UVCCM wilaya ya  wale wa kata zote za jimbo la Kalenga na Isimani limefanyika leo katika  kijiji cha Kalenga na  kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali  akiwemo kamanda  huyo wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw Asas huku wengi  wakihoji  sababu ya kamanda aliyemaliza muda  wake kutoonekana katika  hafla  hiyo .


Akihutubia katika  hafla  hiyo  kamanda  wa UVCCM mkoa  Bw Asas  aliwataka   viongozi hao  waliochaguliwa kufanya  kazi ya  kuwaunganisha  vijana   wote  waliopo ndani ya CCM na  wale wa upinzani  kuona  wanajiunga na  CCM ili  kukiwezesha chama  hicho kuendelea  kushika madaraka  zaidi.

Alisema   kuwa kazi ya  ukamanda na ulezi wa Chipukizi ni pamoja na kuwajengea misingi imara   vijana hao  ili kuwa kitu  kimoja na  kuendelea  kukipigania chama  kuendelea  kubaki madarakani  daima.


Pia  aliwataka  vijana  kuendelea  kubuni miradi ya kimaendeleo  ili kuweza  kuwa na umoja  imara  wenye  uwezo wa kiuchumi na  kuacha  tabia ya  kudanganyika na  baadhi ya  watu wasio na nia njema na umoja  huo na CCM .

Asas  alisema kwa  kuanza  yeye anawachangia kiasi cha Tsh milioni 3 kama  mtaji  wa  kuibua miradi  ya kimaendeleo  katika  wilaya  hiyo na  kuona   vijana wa jimbo la kalenga na  wale wa jimbo la Isimani  wanaendelea  kubuni miradi zaidi ya  kiuchumia.


" Mimi kama kamanda wa UVCCM mkoa nimeanza kwa kuuchangia umoja  huu  kiasin cha Tsh milioni 3   hivyo naomba kamanda  mteule wa UVCCM wilaya ya Iringa nawe uniunge mkono kwa kuchangia  vijana  hawa  pia na mlezi kuona jinsi ya kuchangia chipukizi ili  hata  siku moja  chipukizi  waweze kutembelea  hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha " alisema Asas

Hata  hivyo  kwa upande wake kamanda wa UVCCM wilaya  hiyo Bi Mtasiwa zaidi ya kuwataka  vijana  kuwa pamoja na  kumpongeza kamanda Arif  Abri kwa kazi nzuri aliyoifanya  hakuweza kuunga mkono  jitihada hizo za Asas  zaidi ya  kushukuru nafasi hiyo .


 Huku kwa upande wake Kiswaga  mbali ya  kupongeza kuteuliwa kushika nafasi hiyo bado aliungana  na mkgeni rasmi  kwa  kujitolea  msaada wa  pikipiki moja kwa ajili ya Chipukizi na  kuahidi kuendelea  kuwa karibu zaidi na vijana hao.

No comments:

Powered by Blogger.