UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA SHIGONGO
Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo.
Hiki ndicho ninachokifahamu mimi ndugu yenu.
Maisha
ni vita, maisha ni mapambano na mtindo pekee wa kukusogeza mbele ni
kupigana! Hata uwe mwema kiasi gani utakuwa na maadui, Yesu alikuwa nao,
Mtume Muhammad alikuwa nao, Mandela alikuwa nao na hata Mahatma Gandhi
alikuwa nao.
Hata
ufanyeje maadui watakuwepo tu, utapingwa, utapuuzwa, hivyo basi kamwe
usijaribu kuwafurahisha watu, eti unafanya vitu ili watu wakupende,
utapoteza muda wako bure.
Kumbuka
kuwafurahisha watu ndio barabara kuelekea kwenye umasikini, siku zote
fanya kitu ambacho moyo wako unaridhishwa nacho. Watu watakucheka,
watakutukana matusi yote lakini mwisho wa siku kama ukiendelea mbele hao
ndio watakuja kukupa mkono wa hongera pale utakapoibuka mshindi.
USHUHUDA
WANGU; Kwa miaka yote kumi na tano ambayo nimeishi na kufanya kazi Dar
es Salaam, nimetukanwa sana, nimeitwa majina yote mabaya, nimehukumiwa
sana. Badala ya kuwachukia walionitukana na wanaonitukana (hivi sasa
wakisoma ) ambacho mimi hufanya ni kuziba masikio na kuyachukua matusi
yao kama hamasa kisha kusonga mbele.
Najua
wapo watakaolia pindi nitakapokufa, lakini pia wapo watakaofurahi na
kufanya sherehe kwamba nimekufa, cha muhimu kwangu ni urithi
nitakaouacha hapa duniani baada ya mimi kuondoka, si urithi wa mali bali
idadi ya watu ambao Mungu atasikia sauti zao wakisema "Mtu yule alikuwa
mwenye dhambi lakini alisaidia kutupa tumaini na maisha yetu
yakabadilika."
Hao wakiwa wengi itanitosha, yawezekana sauti zao zitamfanya Mungu aniangalie kwa jicho la huruma na kusema “KARIBU MWANANGU.”
Hao wakiwa wengi itanitosha, yawezekana sauti zao zitamfanya Mungu aniangalie kwa jicho la huruma na kusema “KARIBU MWANANGU.”
Nawatakia
mwaka mpya wenye mafanikio, kumbukeni katika nchi hii ukifanya kazi kwa
nguvu na ukiwa na malengo nafasi ya kufanikiwa ipo bila kujali historia
ya maisha yako.
NAMUOMBA MUNGU MWAKA HUU
UWE WA MPENYO KWA KILA MMOJA WETU.
Asanteni Mungu awabariki
Eric Shigongo James
Mkurungenzi Global Publishers Ltd
No comments:
Post a Comment