MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA WATOTO YATIMA
Mbunge wa Mufindi
Kusini Menrad Kigola akizungumza na mmoja wa watoto waishio katika
mazingira hatarishi katika kituo cha itulituli.(picha zote na Denis Mlowe)
Mbunge wa Mufindi Kusini
Menrad Kigola akiwa katika sherehe za mwaka mpya 2014 na watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi jijini
========= ======== =========
NG’O
WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA WATOTO YATIMA
Na Denis
Mlowe,Mufindi.
WAKURUGENZI
wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoanzishwa kwa lengo la kuhudumia
jamii na hasa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu nchini
wametakiwa kutimiza malengo ya uanzishwaji wa mashirika hayo kwa kuwanufaisha
walengwa badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini (CCM) Menrad Kigola wakati
wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi
laki 7 kwa kituo cha watoto yatima na wale wanaoishi ktk mazingira magumu wa
kituo cha Ifulifuli kilichopo wilaya Mufindi mkoani Iringa na kuongeza kuwa
kumekuwa na utitiri wa NGOs ambazo zimekuwa zikipata mamilioni ya pesa kutoka
kwa wahisani lakini badala ya kuwasaidia walengwa waliokusudia pesa hizo huishia
kuwanufaisha watu wachache kwa manufaa yao binafsi.
Kigola ambaye pia alipata wasaa wa kula chakula cha mchana na watoto hao kwa
lengo la kuukalibisha mwaka mpya amewataka watoto yatima kote nchini kutojiona
wa thamani ya chini kufutia maswaibu wanayoyapitia na badala yake kuwekeza muda
wao mwingi kusoma hali itakayosaidia Taifa kuwa na hazina kubwa ya
wasomi ktk siku za usoni.
Alisema
imekuwa ni kawaida ya baadhi ya asasi zinazolea watoto yatima kutumia misaada
wanayopatiwa kwa manufaa ya waanzilishi kuliko malengo halisi ya asasi hizo.
“Kuna baadhi yenu mmekuwa mnaanzisha asasi kwa lengo la kuwanyonya watoto
yatima hakika haimpendezi mwenyezi MUNGU kuwatumia watoto yatima kwa manufaa
yenu” alisema Kigola
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho kinachomilikiwa na kikundi cha MPENDE
JIRANI,Wilson Ngogi ameitaka serikali kupitia vyombo vyake kuweka mikakati
madhubuti itakayosaidia kubaini mashirika yanayokwenda kinyume na sheria na
taratibu za uanzishwaji wake.


No comments:
Post a Comment