Header Ads

Maalim Seif aweka jiwe la msingi Skuli ya Msingi Tumbe




 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif akihutubia katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika skuli ya msingi Tumbe
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Juma Shamuhuna, akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi skuli ya msingi Tumbe.
Mwalimu wa skuli ya Tumbe akisoma risala ya skuli hiyo. (Picha na Salmin Said, OMKR
 
 
Na Hassan Hamad OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu hatua ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuweka mikakati imara ya kukabiliana na matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini.
 
Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kuasi kikubwa kukabiliana na matatizo ya sekta hiyo yakiwemo upungufu wa vikalio na vitabu vya kusomea.
 
Mhe. Maalim Seif ameeleza hayo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la madarasa manane la skuli ya msingi Tumbe, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Amesema tangu kufanyika kwa Mapinduzi hayo, Wizara ya Elimu imekuwa ikifanya juhudi za kuondosha matatizo hayo, lakini mikakati iliyopo sasa inaweza kumaliza matatizo hayo.
 
Aidha amewapongeza wananchi wa Tumbe na Micheweni kwa moyo wao wa kujitolea, pamoja na mwamko walionao katika  kuchangia huduma za elimu.

No comments:

Powered by Blogger.