MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA WATUMISHI WA HOSPITALI KUU YA MKOA KUSKILIZA KERO ZAO KWA AJILI YA KUZIPATIA UFUMBUZI

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao na
watumishi wa idara ya afya wa hospitali kuu ya Mkoa iliyopo katika
Manispaa ya Sumbawanga. Alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kusikiliza
kero, malalamiko pamoja na ushauri kwa ajili ya kuboresha huduma na
utendaji katika hospitali hiyo. Kero mbalimbali zilitolewa ikiwepo
upandishwaji wa vyeo kuchukua mda mrefu, kubadilishiwa muundo wa vyeo na
kusababisha kupungua kwa mishara kimakosa, uhaba wa vitendea kazi
pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji ambapo kwa sasa hamna hata mmoja.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya kusikiliza kero
mbalimbali aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kutatua kero zilizo chini
ya uwezo wao na zile nyingine kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa
kuzishirikisha mamlaka husika. Kushoto ni Mganga Mkuu hospitali ya Mkoa
Rukwa Dkt. William Gurisha. Kero nyingi zimeonekana kuibuka kutokana na
uhaba wa fedha za OC kutofika kwa wakati na kwa kiwango kilichopangwa.
Hata hivyo hospitali hiyo imeonekana kujipanga kutumia vyanzo vya mapato
ya ndani kutatua baadhi ya kero hizo.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla akifafanua baadhi ya mambo ya kiutawala katika kikao hicho.

Wajumbe katika kikao hicho.

Mmoja ya wahudumu wa afya akitoa kero yake.Picha na Habari na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment