Header Ads

URUGUAY MBIONI KUHALALISHA BIASHARA YA BANGI.

MONTEVIDEO, Uruguay : Serikali ya Uruguay imeonekana ipo mbioni kuhalallisha soko  la Bangi kuweza kufanyika na kutumiwa katika nchi hiyo isipokuwa kwa wanafunzi, watu wenye matatizo ya akili na watu walioathirika na madawa.
Bunge la nchi hiyo tayari limepanga kufanya mdahalo maalum utakaofanyika siku ya jumanne kwa ajili ya kujadiliana uhalalishaji wa biashara hiyo ambayo inapingwa vikali  na karibia nchi zote Duniani, wabunge wa nchi hiyo tayari wameshapitia vifungu vyote vinavyohusu kuhalalisha biashara hiyo hivyo basi kinachosubiriwa cha mwisho ni kura za wabunge hao ambazo zitatoa jibu kamili.
Rais wa nchi hiyo, Jose Mujica(78) alinukuliwa akisema kwamba ”nchi yake haipo kwa ajili ya kupigia debe matumizi ya bangi ila ni kwa lengo la kudhohofisha biashara za wafanyabiashara haramu wa madawa ya kulevya(Bangi)”, hivyo hivyo kwa raia wa nchi hiyo waliweza kutoa maoni yao akiwemo raia mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Marcelo Vazquez aliuambia mtandao wa The Associated Press kwamba hata kama serikali yake ikihalalisha biashara hiyo hatakuwa tayari kulipia kodi kwani zao hilo limekuwa likitumiwa kinyume na sheria  miaka 20 iliyopita nchini humo.

No comments:

Powered by Blogger.