Home
Habari
HAIJAWAHI KUTOKEA, DUNIA YATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA NELSON MANDELA NCHINI AFRIKA KUSINI.
HAIJAWAHI KUTOKEA, DUNIA YATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA NELSON MANDELA NCHINI AFRIKA KUSINI.
Pichani ni Wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Nelson Mandela wakisonga hatua kwa hatua kuelekea katika Majengo ya Muungano eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Mwanamitindo maarum wa Marekani, Naomi CampBel alishindwa kujizuia baada ya kumwaga machozi wakati akiuaga mwili wa Nelson Mandela.
Viongozi mbali mbali pamoja na raia wa Afrika Kusini wanaendelea kutoa heshma za mwisho kwenye mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela ambao umelazwa kwenye ikulu ya Afrika Kusini mji Mkuu wa Pretoria, ambapo utalala hapo kwa siku tatu.
Mwili ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye jengo la Muungano.
Msafara wenye jeneza la Marehemu uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi siku ya jumatano. Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya Afrika Kusini.
Wananchi walijipanga kando kando ya barabara lilipopitishwa jeneza kama ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Msafara ulipita katika mitaa huku baadhi ya raia wakikimbia pembeni kwenye mstari wa askari wa wanajeshi Mwandishi BBC’s Joseph Winter katika mji wa Pretoria amesema.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya Muungano eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Wanachi, wakuu wa nchi walioalikwa na wageni wengine wa kimataifa watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu aliyefariki alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Wageni hata hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.
Leo jioni wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini watashiriki katika tamasha maalum la kumuenzi Mandela na ambalo wananchji wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo.
Marehemu Mandela atazikwa nyumbani kwake katika kijiji Qunu katika jimbo la Cape Mashariki siku ya jumapili.
Maelfu ya raia wa Afrika ya kusini hapa jana waliungana na viongozi mbali mbali duniani katika ibada ya kumbu kumbu siku ya jumanne kama sehemu ya mfululizo wa maombolezo kifo chicho.
Rais wa sasa wa afrika Kusini, Jacob Zuma akiwa ameambatana na mjane wa Mzee Mandela Graca Michael aliyevalia gauni jeusi wakielekea kutoa heshima za mwisho.
Winnie Mandela akilia kwa uchungu wakati akiutazama mwili wa aliyekuwa mume wake, Nelson mandela ukiwa katika Jeneza.
Jacob Zuma akitoa heshima zake za mwisho .
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akielekea kutoa heshima za mwisho.
HAIJAWAHI KUTOKEA, DUNIA YATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA NELSON MANDELA NCHINI AFRIKA KUSINI.
Reviewed by crispaseve
on
8:16 AM
Rating: 5
No comments:
Post a Comment